Tarehe 20/11/2025, KCJE Ltd tumepokea ugeni kutoka CRDB Bank katika ziara maalum ya kuona shehena za viuatilifu na magunia yaliyowasilishwa na kampuni ambazo zimepatiwa mikopo na benki hiyo.
Ziara hiyo ilihusisha ukaguzi wa shehena kutoka kwa wazabuni wanaoshirikiana na KCJE Ltd katika kusambaza pembejeo muhimu zinazowawezesha wakulima kuongeza uzalishaji—hususan kwenye zao la korosho.
Akizungumza kwa niaba ya KCJE Ltd, Kaimu Afisa Masoko Bw. Mathew Rajabu, aliishukuru CRDB kwa kuendelea kutoa mikopo inayowawezesha wazabuni kuleta bidhaa kwa wakati. Ushirikiano huu unaimarisha mnyororo wa thamani na kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.









