KCJE Ltd Yapokea Ugeni wa Maafisa wa Ushirika kutoka Wizara ya kilimo

whatsapp image 2025 12 04 at 09.35.46

Maafisa wa Ushirika kutoka Wizara ya Kilimo wametembelea Ushirika wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Korosho (KCJE Ltd) kwa lengo la kuangazia na kukagua mnyororo wa upokeaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo, viuatilifu pamoja na magunia kwa wakulima wa korosho.

Katika ziara hiyo, maafisa hao walipata fursa ya kujionea kwa karibu mfumo unaotumiwa na KCJE Ltd katika kupokea, kuhifadhi na kusambaza pembejeo na vifaa muhimu kwa wakulima kupitia vyama vikuu vya ushirika. Lengo kuu likiwa ni kuhakikisha huduma hizo zinafika kwa wakati, kwa uwazi na kwa ubora unaokidhi viwango vinavyotakiwa.

Ziara hiyo pia ilihusisha majadiliano kuhusu changamoto zinazojitokeza katika mnyororo wa usambazaji wa pembejeo pamoja na mikakati ya pamoja ya kuboresha huduma hizo ili kuongeza tija katika uzalishaji wa korosho.


Mradi wa Ushirika wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya korosho (KCJE Ltd) unaendelea kudhihirisha mchango wake mkubwa katika kuimarisha ushirika, uchumi wa wakulima, na maendeleo ya Taifa.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *