Katika kuadhimisha msimu wa sikukuu, kampuni ya ROTAI—ambayo ni miongoni mwa wazabuni wakubwa na wa kuaminika wa mizani za kidigitali nchini—imekabidhi zawadi maalumu za Krismasi na Mwaka Mpya (Merry Christmas and Happy New Year) kwa KCJE Ltd.

Zawadi hizi zimewasilishwa kama ishara ya kuthamini ushirikiano mzuri na wa muda mrefu uliopo kati ya ROTAI na KCJE katika utekelezaji wa majukumu ya kusambaza mizani za kidigitali kwenda katika vyama vikuu vya ushirika nchini. ROTAI imeendelea kuwa mshirika muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa mizani za kisasa, bora na zenye viwango vya kimataifa kwa ajili ya kuboresha uadilifu na ufanisi katika mifumo ya upimaji mazao.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, mwakilishi wa ROTAI alitoa shukrani kwa ushirikiano mzuri kutoka KCJE na kusisitiza dhamira ya kuendelea kuboresha huduma kwa lengo la kusaidia sekta ya kilimo na biashara nchini. Kwa upande wao, KCJE imetoa pongezi kwa kitendo hicho cha kiungwana, na kuahidi kuendeleza kazi kwa weledi, uwazi na ubora kama ilivyo desturi ya kampuni.

Tunawatakia wanachama, washirika na wadau wote Krismasi Njema na Mwaka Mpya wenye mafanikio, amani na baraka tele.






