Leo tarehe 19 Desemba, 2025, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa zawadi kwa Ushirika wa Mradi wa Pamoja wa Korosho (KCJE Ltd) kama sehemu ya kuimarisha ushirikiano mzuri kati ya taasisi ya ukusanyaji wa mapato na walipa kodi wake.

Hatua hiyo imelenga kutambua na kuthamini juhudi za KCJE Ltd katika kutekeleza wajibu wake wa kikodi kwa uaminifu, pamoja na kuhamasisha utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati. TRA imeeleza kuwa ushirikiano mzuri na walipa kodi ni nguzo muhimu katika kuhakikisha mapato ya Serikali yanaimarisha utoaji wa huduma za kijamii na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, uongozi wa KCJE Ltd umeishukuru TRA kwa kutambua mchango wa ushirika huo, na umeahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na mamlaka husika katika kutekeleza wajibu wa kikodi na kuzingatia sheria za nchi.


Tukio hilo linaonesha wazi dhamira ya KCJE Ltd kuwa mdau muhimu katika ujenzi wa uchumi wa taifa kupitia sekta ya korosho, sambamba na kuimarisha mahusiano chanya kati ya taasisi za umma na sekta ya ushirika.








