TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA TANO WA KAWAIDA WA USHIRIKA WA MRADI WA PAMOJA WA KOROSHO (KCJE) LTD

logo

MWENYEKITI WA BODI YA USHIRIKA WA MRADI WA PAMOJA WA KOROSHO (KOROSHO COOPERATIVE JOINT ENTERPRISE LTD) KWA NIABA YA BODI, ANAWATANGAZIA WANACHAMA MKUTANO MKUU WA KAWAIDA WA KUSOMA MAPATO NA MATUMIZI PAMOJA NA KUPITISHA MAKADIRIO YA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA MWAKA WA FEDHA 2026/2027, SIKU YA TAREHE 02.07.2026 SAA 03:00 ASUBUHI KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA TIFFANY MTWARA.

WAJUMBE WAWILI WA KILA CHAMA MWANACHAMA WANAOMBWA KUHUDHURIA BILA KUKOSA. MWENYEKITI PIA ANAWAALIKA MAMENEJA WA VYAMA VIKUU WANACHAMA.


AGENDA ZA MKUTANO MKUU WA 5 WA KCJE LTD

1. KUSOMA TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA TANO (5).

2. KUTHIBITISHA AKIDI.

3. KUMCHAGUA MWENYEKITI WA MKUTANO.

4. KUSOMA NA KUTHIBITISHA MUHTASARI WA MKUTANO MKUU WA NNE ULIOFANYIKA TAREHE 21.07.2025.

5. KUJADILI YATOKANAYO NA MKUTANO MKUU WA NNE ULIOFANYIKA TAREHE 21.07.2025.

6. TAARIFA YA MWENYEKITI WA BODI.

7. KUSOMA NA KUPITISHA RASIMU YA MAKADIRIO YA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA MWAKA WA FEDHA 2026/2027.

8. KUSOMA TAARIFA YA UKAGUZI KUTOKA KWA MKAGUZI WA NJE (COASCO) KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025.

9.

(i) KUKASIMISHA MADARAKA YA MKUTANO MKUU KWA BODI KWAAJILI YA KUHUISHA RANDAMA YA MAKUBALIANO (MOU) BAINA YA BODI YA KOROSHO TANZANIA (CBT) NA KCJE LTD JUU YA SHUGHULI ZINAZOHUSU PEMBEJEO NA VIFUNGASHIO VYA ZAO LA KOROSHO NA USIMAMIZI WA AKAUNTI ZA AGRICULTURAL LEVERAGE FUND (ALF)

(ii) KUPOKEA, KUJADILI NA KUPITISHA MAREKEBISHO YA MASHARTI YA KCJE LTD

(iii) KUPITISHA RASIMU ZA MIONGOZO MBALIMBALI YA KCJE LTD AMBAYO NI:

  1. MUONGOZO WA TEHAMA
  2. SERA YA UWEKEZAJI
  3. MUONGOZO WA MAWASILIANO
  4. SERA YA KUJILINDA NA UTAKATISHAJI FEDHA
  5. MABORESHO YA SERA ZA UTUMISHI, UHASIBU NA MANUNUZI
  6. SERA YA KUMLINDA MTOA TAARIFA
  7. SERA YA ELIMU NA MAFUNZO

10. KUTEUA MKAGUZI WA NJE WA HESABU.

11.

MENGINEYO KWA IDHINI YA MWENYEKITI.

(MWISHO WA KUPOKEA MENGINEYO NI TAREHE 30 JUNI 2026 SAA SABA MCHANA).

12. KUFUNGA MKUTANO.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *