Leo katika ofisi za KCJE Ltd, tumepokea wageni kutoka MAT Technology wakiambatana na TCDC kwa ajili ya kuwasilisha teknolojia ya kisasa ya matumizi ya drone (ndege nyuki) katika kilimo cha korosho.
KCJE Ltd imeshiriki kikao, kilichofanyika katika ukumbi wa Tiffany Diamond Hotel, Mtwara.
Katika kikao hicho, wataalamu kutoka MAT Technology waliwasilisha matumizi ya teknolojia ya drone (ndege nyuki) katika sekta ya kilimo cha korosho. Waliwasilisha maelezo ya kitaalamu yakifuatana na video za uoneshaji pamoja na kuwasilisha vifaa (drone) hizo kwa washiriki ili kuzifahamu kwa ukaribu.
Lengo la kikao hiki ni kuendelea kufungua upeo juu ya matumizi ya teknolojia bunifu katika kuongeza ufanisi na tija kwenye uzalishaji wa korosho.
KCJE Ltd inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutafuta na kupokea suluhisho za kisasa zitakazosaidia kukuza sekta ya korosho na kuleta manufaa kwa wadau wote.









