Katika kipindi hiki cha maandalizi kuelekea msimu wa korosho, Mwenyekiti wa Bodi ya Wajumbe wa Korosho Cooperative Joint Enterprise Ltd (KCJE), Ndugu Odas Odas, akiwa ameambatana na Afisa Masoko wa KCJE, Ndugu Methew Rajab, wamefanya ziara maalum katika maghala ya kuhifadhia vifungashio na viuatilifu yaliyopo Wilaya ya Masasi, Mkoa wa Mtwara. ๐ Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kufuatilia kwa karibu hali ya upatikanaji pamoja na viwango vya vifungashio na viuatilifu vilivyopo kwa sasa, ili kuhakikisha maandalizi ya msimu wa korosho yanafanyika kwa ufanisi na kwa wakati. KCJE inaendelea kujizatiti kuhakikisha wakulima wanapata huduma bora na vifaa vinavyokidhi viwango, kwa lengo la kuimarisha mnyororo wa thamani wa zao la korosho nchini.