Wajumbe wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika wa Korosho KCJE LTD Wafanya Ziara ya Mafunzo Tabora
Wajumbe wa mradi wa vyama vikuu vya ushirika wa korosho kupitia KCJE LTD wametembelea chama kikuu cha ushirika cha IGEMBENSABO LTD kilichopo mkoani Tabora, kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika uendeshaji wa vyama vya ushirika.
Ziara hiyo ilikuwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha ufanisi wa mradi wa vyama vya ushirika wa korosho unaosimamiwa na KCJE LTD, ambao kwa sasa unaendelea kufanya vizuri katika kuinua kilimo cha korosho kwa wanachama wake.
Katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo, mradi huo umefanikiwa kuagiza pembejeo muhimu za kilimo kwa ajili ya wakulima wa korosho, hatua ambayo imeboresha uzalishaji na kuinua kipato cha wakulima.
No media files associated with this post.