Uongozi wa Korosho Cooperative Joint Enterprise Ltd (KCJE Ltd) unapenda kutoa salamu za Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya kwa wanachama wote, wadau, washirika wa maendeleo, na watu wote kwa ujumla.
Tunatoa shukrani za dhati kwa ushirikiano, uaminifu na mchango wenu katika kuendeleza sekta ya korosho na kuimarisha shughuli za ushirika kwa mwaka mzima uliopita.
Tunawatakia Krismasi njema, Mwaka Mpya wenye mafanikio, amani, afya njema na maendeleo endelevu.
KCJE Ltd inaendelea kujizatiti katika kutoa huduma bora na kuongeza thamani katika mnyororo wa thamani wa zao la korosho kwa manufaa ya wanachama na Taifa kwa ujumla.

