KCJE YATANGAZA ZABUNI YA UJENZI WA JENGO LA OFISI

zauni

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Cooperative Joint Enterprise Limited (KCJE Ltd), Odas Mpunga, ametangaza zabuni Na. KCJE/2026/2027/W/01 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya KCJE ya ghorofa tano katika eneo la Mtwara Mjini.

Zabuni hiyo inalenga wakandarasi wenye sifa waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), Daraja la I katika ujenzi wa majengo.

Waombaji wanatakiwa kununua kabrasha la zabuni na kuwasilisha maombi yao katika Ofisi za KCJE yakiwa na nakala moja (1) halisi na nakala mbili (2) za kivuli.

whatsapp image 2026 09 01 at 6.16.58 am (1)

Waombaji wanatakiwa kulipa ada isiyorejeshwa ya Sh10,000,000 kupitia akaunti ya CRDB Na. 0150771321300, yenye jina KOROSHO COOPERATIVE JOINT ENTERPRISE LIMITED.

Mwisho wa kuwasilisha zabuni ni Jumatatu, Oktoba 5, 2026 saa 5:00 asubuhi.

Ufunguzi wa zabuni utafanyika siku hiyo hiyo ya Oktoba 5, 2026 katika Ukumbi wa Eden Beach House, Mtwara, mbele ya wawakilishi wa wazabuni watakaokuwepo.

Aidha, baada ya kulipia kabrasha la zabuni, risiti inapaswa kutumwa kupitia barua pepe za ofisi zilizoainishwa kwenye tangazo pamoja na mawasiliano ya upatikanaji wa kabrasha hilo.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *