Hii hapa ratiba ya minada yote ya korosho kwa msimu wa 2026/27, ikihusisha vyama wanachama sita wa KCJE, katika maeneo mbalimbali.
Mnada wa kwanza utafanyika Oktoba 12, 2026 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, chini ya Chama Kikuu cha MAMCU.
Baada ya hapo, minada itaendelea kwa zamu kupitia Vyama Vikuu vya TAMCU, CORECU, TANECU, Lindi Mwambao na RUNALI katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Pwani.
Ratiba hii ya minada itaendelea hadi Januari 22, 2027, ambapo TANECU itafanya mnada wa mwisho katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Newala.
