Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Cooperative Joint Enterprise Limited (KCJE), Odas Mpunga, anautangazia umma kuwa muda wa mwisho wa kuwasilisha zabuni ya ujenzi wa ofisi ya ghorofa tano umeongezwa kwa siku saba.
Zabuni hiyo yenye namba KCJE/2026/2027/W/01, iliyokuwa imepangwa kufungwa Oktoba 5, 2026, sasa itafungwa Oktoba 12, 2026 saa 5:00 asubuhi.
Zabuni hiyo inalenga kumpata mkandarasi atakayetekeleza ujenzi wa ofisi ya ghorofa tano ya KCJE.
Masharti mengine yote ya zabuni yanaendelea kubaki kama yalivyoainishwa katika tangazo la awali.
Waombaji mnatakiwa kuzingatia tarehe na muda mpya wa mwisho wa kuwasilisha zabuni.
